T.I.P KING_FREESTYLE RAP

0:00
0:00
T.I.P KING_FREESTYLE RAP

kabla ya mapinduzi sikiliza hii simulizi itakutia simanzi nikianza kusimulia Tawala za Kiswahili Zikatupiliwa mbali Wakafika majahili Watokao Arabiya Walitumia ujanja Machoni kutia wanja Na kujifanya viranja Usahibu kujitia Wanyonge kitaka kazi Hufanywa ndio wakwezi Wanawake vijakazi Majumbani kueneya Wakipewa kazi ngumu Asofanya mwanadamu Kwao iliwalazimu Viboko kuwalemeya. Alitia ukabila, Mpaka katika kula Asohusu utawala Hana atojipatiya Walokuwa wakaidi Kutomtii Saidi Hawakuipata sudi Viboko liwaingiya. Wengine waliuliwa Mashimoni kufukiwa Sababu wamechukiwa Kutumwa kutoridhiya.  Klabu kazaa mwana Tena aliye mwungwana Na hapo kapewa jina Afrika Asosheniya Ilikuwa jumuiya Ya Wafrika wa Unguja Ilofanya kila njiya Watu kujiingiliya one tisa tatu tano Liundwa umoja huno Jumuiya ilo nono Hadharani kutokeya. Shirav na Afrika Wote wakajumuika Uhasama kuuzika Kheri kujitafutiya Likiwa tarehe tano Ni siku ya Muungano Ni siku iliyo nono Daima twakumbukiya Mwezi Mfungo pili Wa Februari kamili Ziliungana kikweli Hizi mbili jumuiya Mwaka hamsini na saba Ni mwaka wa matilaba Yalipozidi mahaba Afro na Shiraziya. Uovu kila namna Nchini haupo tena Watu wote wapendana Imani imeeneya hongera dr sheni chama kinakuaminia maendeleo visiwani mengi ushatufanyia miundo mbinu ya barabara miundo mbuni ya kilimo miundo mbinu ya bandari miundo mbinu ya utalii miundo mbinu ya masoko miundo mbinu ya mashule miundo mbinu mahospital kwenye miaka 9 ulokaa twajionea vyote hivi umefanya sababu unatuzimia na mengine kibao ambayo yanaendelea unguja na pemba visiwa twajivunia mapinduzi daima miaka 56 tunafurahia

1 Comments

Leave a comment

Author
7 years ago

See track description ↑

User avatar
273
Total plays
165
Followers
162
Following

You may also like