ndoa na njaa
Ndoa na njaa Nakumbuka miaka kadhaa imeshapita, Tangu nilazimishwe na maisha, Nifunge ndoa na huyu kichaa, Walilazimisha nimuoe njaa japo nilikataa, Lakini wapi waliniweka mtu kati, Kwenye harusi nilikula bati, Waliniomba nimtambulishe mke wangu njaa nika mute, Leo miaka kama ishirini hata mtoto hapati, Kutwa kunipotezea wakati, Na kunamda dagaa hataki, Anataka chisp na mishikaki, Huyu mke magumashi, Anachojua yeye ni kumaliza chambi chambi, Kutoka maghetoni hataki, Kuna wakati namzima na makongoro, Na bapa la konyagi, Asubuhi haifiki tumboni kashatia tena kambi Hii ndoa nililazimishwa na maisha, Sikujua kama mpaka leo tungefika, Miaka kibao ya ndoa vita, Na ndoa inagoma kuvunjika, Nasikia njaa akiolewa hahachiki, hatoki nduki analinda ndoa mpaka mauti, Yuko radhi kuishi na yoyote uwe na ghorofa au nyumba ya makuti, Sema hana mapenzi ya dhati, Hata ukiwa una pesa yeye kukuacha ataki, Anachotaka msosi mezani, Yuko radhi kwenda kudoea kwa jirani, Mke huyu kisilani Anaweza kukugeuza kituko, Ukaranda randa msibani, Ili upate chochote uweke tumboni, Maana akianza kudai hachoki, Hajui kuomba ana force Njaa Ndoa na njaa
You may also like

Leave a comment
See track description ↑