taslimucash
taslimucash

daima moyoni(forever in my heart)

daima moyoni(forever in my heart)

42 Plays

30 Jun 2021

Immortallise my loved ones in songs and pictures. #rip #rapfame #hiphop #rap

2 Comments

Leave a comment

3 years ago

Intro Bwana ametoa km zawadi Bwana ametwaa km ahadi.. Usiseme sana ukakufuru.. Kazi ya Maulana tunashukuru Mbele yetu nyuma yenu.. Na iwe amani kwenye roho za marehemu.. Ahh skia... Verse1: Tunaishi tunaishia/ Na Sio rahisi kuficha hisia/ Ah Imekua halisi halisia/ Mshumaa Acha uishe ukiangazia/ Tumaini hafifu mithili ya mgumba kuzaa/ Moyo mdhaifu moyo unadunda butwaa/ Tia muhuri ile siku ambayo Muumba alitwaa/ Takukumbuka kila siku tukiufunga mtaa./ Hakuishi kwa uoga namlilalia mdogo wangu/ Rest in peace young soldier,tangulia mdogo wangu./ Tangu ndani ya nepi  hadi ndani ya jeneza/ Nimekubeba na utabaki moyoni forever/ Mama analia, anaomboleza mtoto wake/ Mziwanda katangulia kaenda na ndoto zake/ Saba mchana baridi natetemeka/ Baba hajiwezi zaidi anaweweseka/ Maswali kwanini umeenda mapema/ Mpokee consolatha, hatunae tena/ Anh Imekua halisi hadi I wish ingekua njozi/ Nakaza moyo nashindwa kuzuia chozi/ Hook: Hakuishi kwa uoga namlilia mdogo wangu/ rest in peace young solja,tangulia mdogo wangu/ Niliona amani machoni mwako, mara ya mwisho waiona nuru/ Tuliza moyo funga macho, hatimaye umekua huru/ Dahhh😢😪 Verse2: Msumari juu ya kidonda kibichi..tanzia/ Umemchukua na huyu uchungu kwa familia/ Nani wa kuzuia yake mapenzi kutimia/ Haijulikani dakika jiandae kisaikolojia/ Habari mbaya juu ya habari mbaya.. makali haya mateso bila chuki/ Tunashukuru ingawa ulikuwepo, nasi kwa muda mfupi/ Ule ukarimu km mama hisani zako kwa wageni/ Tulikula tukanywa nyumbani kwako bila deni/ Leo imebaki hadithi, tunahadithia/ Zig amekumiss frans anaulizia/ Jeje mpweke kinyonge anaugulia/ Kapoteza zawadi pekee,maishani mwake kujirudia./ Naskia vilio vya kwikwi, kina mama wanapiga vifua/ Kwaheri ndugu rafiki, jeneza linatua/ Ahh Weka udongo ishara ya kuonana mara ya mwisho/ Mpo nasi rohoni daima mpaka paradiso/ Rest in peace!😥

You may also like